Ada: lango lako la afya

Maoni elfu 341
Daraja la maudhui
PEGI 3
10M+
Vipakuliwa
Picha ya skrini
Picha ya skrini
Picha ya skrini
Picha ya skrini

Kuhusu programu hii

Jifanyie mwenyewe na ndugu zako uchunguzi wa afya kwa kutumia Ada Assess, inayopatikana kwenye Ada App.
Ada Assess ni tathmini ya dalili unayoweza kutumia saa 24 kwa siku, siku 7 kwa wiki ili kubaini uwezekano wa visababishi vya dalili zako.
Chochote kinachokusumbua, kuanzia maumivu, maumivu ya kichwa au wasiwasi hadi mzio au kutohimili aina fulani za vyakula, Ada App inayopatikana bila malipo inakupa fursa ya kutumia Ada Assess, ambapo unaweza kupata majibu ukiwa nyumbani kwako.

Inafanyaje kazi?

Unaanza tathmini ya dalili kwa kubofya kitufe kwenye app. Hii inafungua Ada Assess.
Unajibu maswali rahisi kuhusu afya na dalili zako.
Ada Assess inatathmini majibu yako kwa kuyalinganisha na maarifa yake ya kitiba yenye maelfu ya matatizo ya kiafya na hali za kiafya.
Unapokea kutoka Ada Assess ripoti ya tathmini iliyotayarishwa kulingana na hali yako, yenye muhtasari wa uwezekano wa visababishi vya dalili zako na mwongozo kuhusu kiwango kinachofaa cha huduma ya afya.

Unaweza kutarajia nini?

Faragha na usalama wa data – tunazingatia kanuni kali zaidi za data ili kulinda taarifa zako na kuhakikisha zinabaki kuwa za faragha.
Tathmini inayotolewa na kifaa cha kitiba kilichoidhinishwa – tathmini ya dalili, mantiki yake ya kitiba na ripoti vyote vinatolewa na Ada Assess.
Ripoti ya tathmini ya afya – shiriki taarifa muhimu na daktari wako kwa kufikia na kuhamisha ripoti zako za tathmini za awali.

Inapatikana saa 24 kwa siku, siku 7 kwa wiki – unaweza kutumia Ada Assess wakati wowote, mahali popote.

Inapatikana katika lugha 7 – chagua lugha yako na uibadilishe wakati wowote kwenye mipangilio (settings): Kiingereza, Kijerumani, Kifaransa, Kireno, Kihispania, Kiswahili na Kiromania.

Ada App yenyewe si kifaa cha kitiba. Bali inatoa fursa ya kutumia Ada Assess, kifaa cha kitiba cha Ada Health GmbH kilichoidhinishwa na chenye alama ya CE (CE 0123).

Maelezo ya kina kuhusu viwango vyetu vya ubora wa kitiba yanapatikana hapa: [https://about.ada.com/medical-quality/]

TAHADHARI: Ada Assess haiwezi kukupa utambuzi wa ugonjwa (medical diagnosis). Katika hali ya dharura, wasiliana haraka na huduma ya matibabu ya dharura. Ada App si mbadala wa ushauri wa mtaalamu wako wa afya au miadi na daktari wako.

Tungependa kusikia kutoka kwako. Ikiwa una maoni yoyote au ungependa tu kuwasiliana nasi, wasiliana nasi kwa support@ada.com. Maoni yako yatashughulikiwa kwa mujibu wa Sera yetu ya Faragha. [https://ada.com/raw/privacy-policy/]
Pata tathmini ya dalili sasa. Lango lako la afya saa 24/7.
Ilisasishwa tarehe
13 Okt 2026

Usalama wa data

Usalama huanza kwa kuelewa jinsi wasanidi programu wanavyokusanya na kushiriki data yako. Faragha ya data na mbinu za usalama zinaweza kutofautiana kulingana na matumizi yako, eneo ulilopo na umri wako. Msanidi programu ametoa maelezo haya na anaweza kuyasasisha kadiri muda unavyopita.
  • Programu hii huenda ikaruhusu aina hii ya data ikafikiwa na washirika wengine
    Mahali, Taarifa binafsi na nyingine4
  • Programu hii huenda ikakusanya aina hizi za data
    Mahali, Taarifa binafsi na nyingine4
  • Data inasimbwa kwa njia fiche inapotumwa
  • Unaweza kuomba data hiyo ifutwe

Ukadiriaji na maoni

Maoni elfu 335
Obadia Mdolo
4 Juni 2025
Nzuri sana inatumika kama daktari wa dharura wakati wowote ule. asante sana ada.
Watu 6 walinufaika kutokana na maoni haya
Je, maoni haya yamekufaa?
susu Ahmed Agil
25 Juni 2025
sawa
Je, maoni haya yamekufaa?
Daudy lute matiasi
12 Juni 2025
asante kwahuduma nzuri
Watu 6 walinufaika kutokana na maoni haya
Je, maoni haya yamekufaa?

Vipengele vipya

Asante kwa kuitunza afya yako kwa kutumia app ya Ada. Katika sasisho hili, tumerekebisha hitilafu na kuboresha vipengele ili kukuwezesha kuitumia app kwa urahisi. Ikiwa una maswali au maoni, tafadhali wasiliana nasi kupitia support@ada.com.

Usaidizi wa programu

Kuhusu msanidi programu
Ada Health GmbH
support@ada.com
Neue Grünstr. 17 10179 Berlin Germany
+49 30 40367390
Maelezo ya kifaa cha matibabu kinachotumika katika Umoja wa Ulaya
Ada Assess (SRN: DE-MF-000009202)
Ada Health GmbH
Neue Grünstraße 17, 10179 Berlin, Germany
UDI-DI: 04260744820760

Programu zinazolingana