Ratiba ya mwezi, kazi za leo na mazoea yako, vyote kwenye kalenda moja.
Mongle Calendar inakusaidia kupanga miadi na kazi kwa visanduku vya rangi tulivu. Anza bila kufungua akaunti, na uone mipango yako hata bila intaneti.
Panga siku kwa namna yako
• Ona miadi na kazi pamoja kwenye kalenda ya mwezi.
• Bonyeza kisanduku kwa muda ili kukihamisha kwenda siku nyingine.
• Gawanya kazi kubwa katika orodha ndogo. Weka marudio na vikumbusho kwa shughuli za kawaida.
• Hifadhi mambo ambayo bado hayana tarehe kwenye sehemu ya ‘Someday’.
Jenga mazoea kwa mwendo wako
Chagua siku zinazokufaa kusoma au kufanya mazoezi, kisha weka alama ukimaliza. Tumia wijeti kuona kalenda, kazi na mazoea kwenye skrini ya mwanzo.
Ingiza matukio uliyochagua kutoka kwenye kalenda za simu, zikiwemo kalenda za Google zilizounganishwa na simu. Ona siku zilizobaki hadi safari au tarehe muhimu.
Rekodi zinahifadhiwa kwenye kifaa chako. Weka nakala rudufu za ndani kiotomatiki au hamisha na urejeshe faili. Unganisha akaunti ya Google kwa nakala rudufu na urejeshaji kupitia Google Drive. Funga programu kwa nambari ya siri au uthibitishaji wa kibayometriki.
Chagua rangi, fonti na mwonekano angavu au wa giza. Kiolesura cha programu kinapatikana kwa Kiingereza na lugha nyingine 14; Kiswahili bado hakipatikani ndani ya programu.
Sera ya faragha: https://www.mongleharu.com/calendar/privacy/
Msaada: https://www.mongleharu.com/calendar/support/
Kalenda, orodha ya kazi na mazoea. Vikumbusho na wijeti, hata bila intaneti.
Ilisasishwa tarehe
10 Nov 2026